Ukumbusho Wa Swiyaam (Funga) za Ayyaamul-biydhw (Masiku meupe) Jumaadal-Uwlaa 1437H






SWIYAAM (FUNGA) SIKU TATU KILA MWEZI THAWABU ZAKE NI SAWA NA THAWABU ZA SWIYAAM YA MWAKA!

Tunapenda kuwakumbusha Swiyaam (funga) za Ayyaamul-Biydhw (masiku meupe) ambayo ni tarehe 13, 14, 15 katika kila mwezi wa Kiislaam (Hijriyyah). Masiku hayo mwezi huu wa Jumaadal-Uwlaa 1437H, yataangukia tarehe 22, 23, 24 Februari (Jumatatu, Jumanne, Jumatano). Bonyeza 'Endelea' upate fadhila kadhaa za Ayyaamul-Biydhw na fadhila za Swiyaam siku tatu kila mwezi, pamoja na fadhila za Swiyaam kwa ujumla.  Soma  na utekeleze ili ufaidike na ujichumie thawabu tele In Shaa Allaah.  Na hakuna tawfiyq isipokuwa ya Allaah ‘Azza wa Jalla, Kwake tunatawakali na Kwake tunarudia kutubia.


عَنْ أَبي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ:((مَنْ صَامَ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَذَلِكَ صِيَامُ الدَّهْرِ)) فَأَنْزَلَ اللهُ تُصْدِيقَ ذَلِكَ في كِتَابِهِ الْكَرِيمِ: ((مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا))، الْيَوْمُ بِعَشَرَةِ أَيّامٍ. أخرجه أحمد والترمذي وقال حديث حسن ، والنسائي وابن ماجه وابن خزيمة

Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu). Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Yeyote atakayefunga (swiyaam) kila mwezi siku tatu, ni sawa na  swiyaam ya mwaka mzima, kisha Allaah Akateremsha Aayah ithibitishayo hayo: Atakayekuja (Siku ya Qiyaamah) kwa amali nzuri basi atapata (thawabu) kumi mfano wa hiyo))   Siku moja kwa malipo ya siku kumi. [Imepokewa na At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan, An Nasaaiy na Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (4/102)]. Aayah: Surat Al-An’aam (160)


Maana Ya Biydhw:  Yameitwa ‘Biydhw’ (meupe) sababu usiku wa siku hizo hung'aa kutokana na mwanga wa mwezi. Ayyaam Al-Biydhw (Masiku Meupe) tarehe zake ni 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa kalenda ya Kiislamu.

 عَنْ جريرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَن النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيهِ وَسَلَّمَ قَالَ  : ((صِيَامُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ صِيَامُ الدَّهْرِ ، أَيَّامُ الْبِيضِ صَبِيحَةَ ثَلاثَ عَشَرَةَ وَأَرْبَعَ عَشَرَةَ وَخَمْسَ عشَرَةَ))  

Imepokelewa kutoka kwa Jariyr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabii (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Swiyaam (kufunga) siku tatu kila mwezi ni sawa na swiyaam ya mwaka; na masiku meupe ni tarehe kumi na tatu, kumi na nne na kumi na tano [13, 14, 15]))  [An-Nasaaiy (2420)  na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh At-Targhiyb (1040)]


عن أبي ذر رضي الله عنه: قال لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((يَا أَبَا ذَرٍّ ، إِذَا صُمْتَ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَصُمْ ثَلاثَةَ عَشَرَ وَأَرْبَعَةَ عَشَرَ وَخَمْسَةَ))

Imepokelewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: ((Ee Abu Dharr! Endapo utafunga (swiyaam) siku tatu za kila mwezi, basi funga siku ya 13, ya 14, na ya 15)) [Imepokewa na At-Tirmidhiy na kasema Shaykh Al-Albaaniy kuwa ni Swahiyh]

قال صلى الله عليه وسلم: ((أَلا أُخْبِرُكُمْ بِمَا يُذْهِبُ وَحَرَ الصَّدْرِ صَوْمُ ثَلاثَةِ أَيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْر))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je, nikujulisheni jambo litakaloondosha uovu wa moyo? Ni swiyaam (kufunga) siku tatu kila mwezi)) [An-Nasaaiy 2/2386 na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh An-Nasaaiy (2249)]

Asw-Swuyuutwiy (Rahimahu Allaah) amesema katika An-Nihaayah: Uovu wa moyo ni; udanganyifu, wasiwasi, na imesemwa pia ni uhasidi, chuki, na imesemwa pia uadui na imesemwa ghadhabu”

Baadhi ya fadhila nyinginezo za Swiyaam (kufunga)

1- Kuepushwa na Moto masafa ya miaka sabiini.
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : مَنْ صَامَ يَوْماً فِي سَبِيلِ اللَّهِ بَعَّدَ اللَّهُ وَجْهَهُ عَنْ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا .

Imepokelewa kutoka kwa Abu Sa’iydin Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Atakayefunga (swiyaam) siku moja kwa ajili ya Allaah, Allaah Atamweka mbali  uso wake na Moto masafa ya miaka sabiini)) [Muslim 2/208]

Na katika Hadiyth nyengine pia:

عن جابر رضِي الله عنه عن النبيِّ  صلى الله عليه وسلم  قال: ((الصِّيام جُنَّة يَستَجِنُّ بها العبدُ من النار))   

Imepokelewa kutoka kwa  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam  amesema: ((Swiyaam (kufunga) ni kinga itamukoa mja kutokana na Moto [wa Siku ya Qiyaamah])) [Ahmad 2/402, Taz Swahiyh At-Targhiyb 1/411 na Swahiyh Al-Jaami’ 3880]

2- Mwenye kufunga (swiyaam) atafunguliwa mlango wa Rayyaan huko Jannah

عَنْ سَهْلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((إِنَّ فِي الْجَنَّةِ بَابًا يُقَالُ لَهُ الرَّيَّانُ يَدْخُلُ مِنْهُ الصَّائِمُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ يُقَالُ أَيْنَ الصَّائِمُونَ فَيَقُومُونَ لَا يَدْخُلُ مِنْهُ أَحَدٌ غَيْرُهُمْ فَإِذَا دَخَلُوا أُغْلِقَ فَلَمْ يَدْخُلْ مِنْهُ أَحَدٌ ))

Imepokelewa kutoka kwa Sahl  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Hakika katika Jannah kuna mlango unaitwa Rayyaan, wataingia humo siku ya Qiyaamah wenye kufunga (swiyaam), hatoingia yeyote mwingine. Itasemwa: “Wako wapi wenye kufunga (swiyaam)? Watasimama kuingia hatoingia yeyote mwingine, watakapoingia, utafungwa, basi hatoingia mwengine)) [Al-Bukhaariy 1763, Muslim 1947]

3- Swiyaam (kufunga) ni kwa ajili ya Allaah Pekee na anayefunga hupata  thawabu maradufu, furaha mbili; anapofuturu na atakapokutana na Rabb Wake. Na harufu ya mdomo kuliko misk.

عنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعمِائَة ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ فَرْحَةٌ عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفُ فِيهِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu): ((Kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema: Isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga swawm atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Rabb wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk)) [Muslim na Ahmad]

4-Du’aa ya mwenye kufunga (swiyaam) inakubaliwa:

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه)  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاَثَةٌ لاَ تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ,  الإِمَامُ الْعَادِلُ, وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ, وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ ...))

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: (([Watu] Watatu hazirudishwi du'aa zao; Imaam muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na du'aa ya aliyedhulumiwa…..,)) [Ahmad na ibn Maajah. Pia Al-Bayhaqi 3/345 taz pia As-Silsilah Asw-Swahiyhah 1797]

5- Swiyaam (funga) itamuombea itamuombea shafaa mwenye kufunga Siku ya Qiyaamah:

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : ((الصِّيَامُ وَالْقُرْآنُ يَشْفَعَانِ لِلْعَبْدِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، يَقُولُ الصِّيَامُ:  أَيْ رَبِّ مَنَعْتُهُ الطَّعَامَ وَالشَّهَوَاتِ بِالنَّهَارِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ.  وَيَقُولُ الْقُرْآنُ: مَنَعْتُهُ النَّوْمَ بِاللَّيْلِ فَشَفِّعْنِي فِيهِ.  قَالَ : فَيُشَفَّعَانِ))

Imepokelewa kutoka  kwa 'Abdullaah bin ‘Amru  (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa)  kwamba Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Swiyaam (funga) na Qur-aan zitamuombea mja siku ya Qiyaamah, itasema swiyaam: “ee Rabb!  Nimemzuia chakula chake na matamanio wakati wa mchana, basi nnamuombea shafaa, na itasema Qur-aan nimemzuia usingizi wake wakati wa usiku basi nnamuombea shafaa”. Akasema: ((Basi [viwili hivyo] vinaombea shafaa na kukubaliwa]. [Ahmad (174/2) Al-Haakim (1/554), Al-Bayhaqiy (3/181) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaamiy’ 7329]

6- Swiyaam hakuna mfano wake:

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ  قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: مُرْنِي بِأَمْرٍ آخُذُهُ عَنْكَ قَالَ: ((عَلَيْكَ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَا مِثْلَ لَهُ))  

Kutoka kwa Abu Umaamah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimwendea Rasuli wa Allaah Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam nikasema: “Niamrishe jambo [litakalonifaa Aakhirah] nilichukue kwako”. Akasema: ((Shikilia Swawm kwani hakika hakuna mfano wake)) [An-Nasaaiy]

7- Ukifariki ukiwa na Swawm utaingia Jannah nayo ni husnul-khaatimah

 عن حذيفة  رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قَال: ((مَن خُتِمَ له بصيام يومٍ دخل الجنة))

Imepokelewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kutoka kwa Nabiy Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekuwa amali yake ya mwisho kabla ya kufariki ni swawm ataingia Jannah)) [Ahmad 5/391. Taz. Swahiyh At-Targhiyb 1/412, Swahiyh Al-Jaami’ 6224]
Next
This is the current newest page
Previous
Next Post »

1 comments:

Click here for comments
Unknown
admin
April 16, 2022 at 7:57 PM ×

Ukumbusho Wa Swiyaam (Funga) Za Ayyaamul-Biydhw (Masiku Meupe) Jumaadal-Uwlaa 1437H ~ Hd Studio >>>>> Download Now

>>>>> Download Full

Ukumbusho Wa Swiyaam (Funga) Za Ayyaamul-Biydhw (Masiku Meupe) Jumaadal-Uwlaa 1437H ~ Hd Studio >>>>> Download LINK

>>>>> Download Now

Ukumbusho Wa Swiyaam (Funga) Za Ayyaamul-Biydhw (Masiku Meupe) Jumaadal-Uwlaa 1437H ~ Hd Studio >>>>> Download Full

>>>>> Download LINK 2y

Congrats bro Unknown you got PERTAMAX...! hehehehe...
Reply
avatar
Thanks for your comment